ASSAs

NDEGE MPYA MBILI KUTUA LEO ZANZIBAR

50
0
Share:

Na ELISAFI FADHILI

Ndege mpya 2 aina ya Airbus A220-300, zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania zimeondoka nchini Canada kuja Tanzania.

Ndege hizo zitapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume Mjini Unguja, Zanzibar, leo Oktoba 8, 2021 majira ya saa 9:00 Alasiri na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Ndege hizo ambazo zimepewa majina ya Zanzibar na Tanzanite zitakamilisha hesabu ya ndege 11 zilizonunuliwa na kuwasili hapa nchini.

Ndege nyingine 5 (Boeing 787-8 Dreamliner {2}, Airbus A220-300 {2} na Bombardier Dash 8 Q400 {1}) zimeshalipiwa na zitakuja baadaye.
.

(Visited 43 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us