ASSAs

SQUID GAME ILIKATALIWA NA KWA MIAKA 10

24
0
Share:

Makala na Deusdedith Innocent

Onyesho la Squid Game ambalo liliachiwa Septemba 17, likiwa linaonyesha kundi la watu wazima wakijitahidi kulipa madeni yao, wanaalikwa kucheza michezo ya watoto ili kushinda takribani dola milioni 40 lakini kupoteza michezo kuna matokeo mabaya.

Hwang Dong-hyuk, Muundaji na Mkurugenzi wa kipindi hicho, alikuja na wazo mwaka 2009 wakati akiishi na Mama na Bibi yake, lakini ilifika mahali akataka kukata tamaa na kumbidi kuacha kuandika Script na kuwaza kuuza laptop yake ili kupata pesa ya kujikimu kwani Studio zilikataa wazo lake kwa miaka kumi zikidhani kuwa mtindo wake ni mbaya sana na sio wa kweli.

Netflix ilichukua onyesho hilo miaka miwili iliyopita na limeandikwa kwa lugha 31 na kwa sasa ni onyesho pendwa katika nchi zaidi ya 90, na lina asilimia 95 ya watazamaji nje ya Korea Kusini.

Squid Game pia iliandika historia kwa kuwa onyesho la kwanza la Korea kufanya vizuri zaidi ya katika mtandao wa Netflix nchini Marekani.

Hwang alisema anaamini janga la Corona limefanya wazo la onyesho lake kupendeza zaidi kwa studio, ambayo ni Netflix, kwani ilizidisha tofauti za uchumi na uchumi ambazo zinahusika katika mpango wa onyesho.

“Ulimwengu umebadilika, Pointi hizi zote zilifanya hadithi kuwa ya kweli sana kwa watu ikilinganishwa na muongo mmoja uliopita.” Hwang aliiambia The Journal

Minyoung Kim, makamu wa rais wa Netflix aliunga mkono maoni hayo, na kuongeza kuwa onyesho hilo linauliza na kujibu maswali ya maadili juu ya thamani ya mtu.

“Sisi sio farasi, sisi sote ni wanadamu.”

(Visited 14 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us