ASSAs

UJERUMANI YA KWANZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

31
0
Share:

Baada ya ushindi wa jana usiku dhidi ya North Macedonia, Ujerumani limekuwa taifa la kwanza kufuzu kwenda kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani huko nchini Qatar.

Sasa Ujerumani wanaungana na mwenyeji Qatar kuwa timu mbili zilizojihakikishia kucheza kombe la Dunia 2022.

Tuiombee timu yetu ya Taifa Taifa Stars izidi kufanya vizuri ili na sisi twende kushiriki kombe la Dunia Qatar 2022.

Hadi sasa Tanzania inaongoza kundi J ikiwa na pointi saba sawa na Benin wanaoshika nafasi ya pili, Congo wana pointi tano wakiwa nafasi ya tatu na Madagascar wa nne wakiwa na pointi tatu.

Taifa stars bado ina michezo ya marudiano na Congo ambapo mchezo wa awali ulimazika kwa sare na Madagascar ambapo mchezo wa awali Taifa Stars ilishinda.

(Visited 20 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us