ASSAs

WAKUU WA MIKOA HAKUNA KUTOKA NJE YA MIKOA YAO

56
0
Share:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amewapiga marufuku wakuu wa mikoa na wakurugenzi kutoka nje ya mkoa bila kibali cha Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu.

Ummy amesema hayo leo Jumanne Oktoba 12, 2021 katika mkutano wa waandishi wa habari akifafanua Tamisemi itakavyotumia mkopo wa IMF kutekeleza miradi mbalimbali ambayo utekelezaji wake unawahusu viongozi na watendaji hao wa mikoa nchini.

Amesema kuwa wakuu wa mikoa na wakurugenzi wanatakiwa kuepuka safari zisizo za lazima za kutoka nje ya mkoa isipokuwa kwa kibali cha viongozi hao.

“Lakini kwa sababu tunajambo hili kubwa, ninawaelekeza viongozi wote wa Serikali ndani ya Tamisemi, ngazi ya mikoa, wilaya na halmashauri kuepuka safari zisizo za lazima zinazohusu kutoka nje ya mkoa wako isipokuwa kwa kibali cha viongozi wakuu wa nchi.”

“Kwa hiyo mkuu wa mkoa ukitaka kutoka ndani ya Mkoa wako kipindi hiki lazima upate kibali cha rais, kibali cha Makamu wa Rais au Waziri Mkuu

(Visited 54 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us