ASSAs

UKWELI WA WAZIRI MAMBO YA NDANI KUHUSU AJIRA ZA JESHI LA POLISI UNAWAKWAZA?

150
0
Share:

Kelele zinazoendelea mitandaoni kuhusu ajira katika Jeshi la Polisi Tanzania, zinachanganya kidogo!Baada ya ufafanuzi wa Mh Waziri wa mambo ya ndani George Simbachawene watu wengi wanaonekana kuhamaki na kutoa shutuma kwamba ajira zimetoka kwa upendeleo!

Utafiti wangu unaonyesha kuwa kati ya Polisi watano wanaoajiriwa wakiwa na devision I & II,mmoja tu ndio uendelea na kazi za kipolisi huku Askari wanne wakiomba ruhusa na wakati mwingine kulazimisha kwenda kusoma hivyo Jeshi kukosa askari kwa ajili ya kazi za ulinzi!

Katika mwaka wa fedha 2021-2022 kimetia fora kwa kupeleka askari wengi katika kozi ya mkaguzi Msaidizi hivyo kupelekea kuwepo kwa uhaba mkubwa wa Askari wa chini!

Inasemekana kati ya wahitimu zaidi ya 2000+ waliomaliza kozi ya ukaguzi msaidizi juzi katika Chuo cha Taaluma za Polisi Moshi,zaidi ya robo tatu walikuwa na Shahada ya kwanza,pili na PhD! Je,kwa idadi hii ya askari kutoka NCO’s kwenda Ukaguzi msaidizi,Je,nani atalinda Banki,nani atalinda raia,mahakamani,mahabusu na kazi zinginezo za kipolisi?Kiutaratibu Askari wa ngazi ya ukaguzi msaidizi hapaswi kukaa katika malindo!

Anachosema hapa Mh Waziri ni rahisi sana,hakuna devision I & II ambaye atakubali kutojiendeleza kutokana na ufaulu huo lakini ni ngumu mno kwa askari aliyepata divisheni IV ya mwisho mwisho kuamua kwenda shule!Polisi wanaongea haya kwa takwimu zao walizonazo kama unabisha endelea kubisha,ukweli wanaujua wao!

UKWELI UKOJE KUHUSU AJIRA ZA POLISI?

1.Jeshi la Polisi kwa sasa linaweza likawa linakabiliwa na upungufu wa askari wa kada ya chini yaani NCO’s kwa sababu ambazo Mh Waziri kashazisema awali!Hawa jamaa kwa Sasa wamejazana Kwenye vyuo vikuu wakitafuta degree ambazo nyingine hazina manufaa ya moja kwa moja na Jeshi!Mfano,mtu mwenye degree ya kilimo anasaidiaje Jeshi la Polisi?

2.Watu wanapaswa kujua kuwa upolisi ni taaluma kama taaluma zingine kwahiyo kitendo cha Askari wengi kukimbilia kusoma kozi za kiraia sio tu hazilisaidii Jeshi husika kutimiza malengo ya kulinda raia na mali zao!

Ingekuwa vyema Askari hawa wangekuwa wanasoma kozi ambazo zinaweza kusaidia kutekeleza majukumu yao mfano,kozi za “Security Management,Investigation na Operations” ambazo zinapatikana kupitia mitandao katika vyuo vikuu vya nje ya Nchi mfano Chuo Cha “International Security Management Institute” cha Uwingereza!

4.Kwanini vijana wetu wasiende kusoma kwanza katika ngazi ya fomu high level kama wana ufaulu mzuri baadae kwenda katika vyuo vikuu?Kwanini vijana wanataka kukatiza ndoto zao?!Je,wanataka ajira au wanataka shule au wanataka wapate ajira baadae watangaze kwenda kusoma?,nani atalinda banki zetu na mali zetu?

Jeshi sio kampuni kama Banki ambayo inaweza kuhitaji wasomi kuanzia kada ya chini mpaka ya kada ya juu!Jeshi kwa malengo maalum lazima liwe na kada za askari wa darasa la saba,four,six na vyuo vikuu!Ajira za Jeshi uamuliwa na mahitaji ya Jeshi husika na sio kwa matakwa ya watu wa mitandaoni!

5.Leo nimestuka kidogo,hawa vijana wenye ufaulu huu wa divisheni I & II lini wameanza kulipenda Jeshi la Polisi?wanataka ajira au kweli wanawito wa kuwa askari?,wakumbuke kuwa uaskari sio ajira bali uaskari ni kazi ya kuuza roho yako kwa ajili ya Watanzania!

Nidhamu ya askari ujengwa katika misingi mingi kwahiyo tuawachie Askari wenyewe waamue ni aina gani ya Askari wanawataka kwa sasa na tuache siasa za mitandaoni kwa sababu ya kusaka ajira!Jeshi la Polisi hakiwezi kuajiri kila mwenye division I,II,III,IV kwani kuna ambao wana devisheni IV wapo wengi waliokosa!

Bado Mh Rais Samia ataendelea kutoa ajira katika majeshi ya Magereza,Uamiaji,Zimamoto na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ni suala la kusubili tu labda kesho yenu ni nzuri zaidi ya leo!

George Michael Uledi.

(Visited 94 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us