ASSAs

SUDANI HALI SI SHWARI

134
0
Share:

Watu Saba wauawa na wengine 140 kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Sudan.

Marekani imesitisha msaada ya karibu Dola Milioni 700 kwenda Sudan ikitishia viongozi wa mapinduzi ya kijeshi kurejesha Serikali iliyopinduliwa.

Msaada huo ulilenga kusaidia Wasudani ambao wapo katika kipindi cha mabadiliko ya utawala wa Kidemokrasia tangu alipoondolewa Omar Bashir mnamo 2019.

Lakini mabadiliko hayo yameingia katika sura mpya baada ya Afisa wa Jeshi Abdel Fattah Al-Burham kuongoza jeshi na kumtia mbaroni waziri mkuu Abdallah Hamdok na mawaziri wengine.

Al Burham ametangaza kwamba Jeshi pekee ndio itachukua hatamu ya uongozi kwa kipindi chote mabadiliko baada ya kuvunja Serikali iliyokwepo.

(Visited 33 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us