ASSAs

RAIS SAMIA AELEKEA CAIRO MISRI

217
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Novemba 10,2021 ameondoka nchini kuelekea Cairo Misri kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu ambapo ziara hii ya Kiserikali inafuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Abdel Fatah Al Sisi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kabla ya kuondoka nchini kuelekea Cairo, Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati akielekea kupanda Ndege kwenda Cairo, Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliomsindikiza katika uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati akielekea Cairo nchini Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

(Visited 37 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us