ASSAs

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SANJAY DUTT

102
0
Share:Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na muigizaji mashuhuri wa filamu za Kihindi kutoka nchini India, Sanjay Dutt ambaye ameahidi kushirikiana na Serikali katika kukuza tasnia ya filamu nchini.

Amekutana na msanii huyo leo (Jumatano, Novemba 10, 2021) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema Serikali itampa ushirikiano wote kuhakikisha msanii huyo anatimiza malengo ya ziara yake nchini.Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa filamu nchini kutumia ujio wa msanii huyo mkubwa duniani kuimarisha uhusiano pamoja na kujifunza namna bora ya kuboresha kazi zao kupitia yeye na kuweka mipango ya kufanyakazi kwa pamoja.

Pia, Waziri Mkuu amemshukuru msanii huyo ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania katika kuendesha mafunzo ya masuala mbalimbali katika tasnia  hiyo  ikiwemo uandaaji wa filamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa hususani kwa vijana.Naye, Dutt amesema amevutiwa na fursa nyingi zilizoko kwenye sekta ya utalii nchini na kwamba ameahidi kuvitangaza vivutio hivyo na kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kwenye ramani ya dunia katika masuala ya utalii.

Wakati huo huo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema kupitia ujio wa Dutt, Wizara inategemea kuangalia maeneo ya kimkakati ambayo wanaweza kushirikiana na msanii huyo ikiwemo uandaaji wa filamu, kuongeza wigo wa masoko ya filamu na matumizi ya teknolojia katika kuikuza sekta ya filamu nchini.

Aliongeza kuwa kupitia Chuo cha Sanaa Tanzania (TaSUBa) Dutt ametoa ushauri wa namna bora ya kushirikina ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasanii na waandaaji  wa filamu “Lengo letu ni kuhakikisha wasanii wetu wanatengeneza filamu ambazo zitakuwa na viwango vya kimataifa na ameahidi kuwaleta wataalamu ili wawasaidie wasanii wetu

(Visited 26 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us