ASSAs

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MPYA

567
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Dkt. Florence Martin Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).

2. Amemteua Prof. Sylvia Shayo Temu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).

3. Amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC).

4. Amemteua Dkt. Mwamini Madhehebi Tulli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

5. Amemteua Bw. Jacob Jail Kibona kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

6. Amemteua Dkt. Irene Charles Isaka kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

7. Amemteua Dkt. Tumaini Katunzi kuwa Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).

8. Amemteua Bw. Godfrey Basilo Mbanyi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

Uteuzi wa Viongozi hao umeanza Novemba 9, 2021.

@lemutuz_tv @lemutuz_superbrand
#lemutuzUpdates

(Visited 214 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us