ASSAs

AKAMATWA KWA KUBAKA NGURUWE

78
0
Share:

Njombe: Mkazi wa kijiji cha Mavanga, Wilayani Ludewa Mkoani Njombe Afro Nyigu ( umri miaka 31) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka Nguruwe.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Ramadhani Kihanga akielezea tukio hilo amesema kuwa, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 14, 2021 ambapo Mtuhumiwa huyo alifika katika machinjio ya nguruwe huku akiwa amelewa na kukuta Nguruwe akiwa amefungwa kamba kwa maandalizi ya kuchinjwa ndipo alivua nguo kisha akamvamia nguruwe na kufanya nae mapenzi.

Wakati akiendelea na tendo hilo mlinzi wa machinjio hiyo alikuwa ametoka kidogo na aliporejea alimkuta kijana huyo akiendelea kufanya kitendo hicho ambapo alimkamata na kumpigia simu Balozi wa Mtaa na Mtendaji wa Kijiji ambao walifika katika eneo hilo la tukio.

Ameongeza kuwa, walipomuhoji kijana huyo sababu za kufanya kitendo hicho alidai ni maamuzi yake binafsi hivyo hapaswi kuulizwa, Viongozi wamemchukua na kumkabidhi mikononi mwa Polisi.

@lemutuz_tv @lemutuz_superbrand

lemutuzUpdates

(Visited 21 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us