ASSAs

WANAFUNZI WAJAWAZITO KUENDELEA NA SHULE

83
0
Share:

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari watakaokatisha masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, mimba na changamoto mbalimbali za kifamilia watapewa fursa ya kurejea Shuleni katika mfumo rasmi.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hii leo Novemba 24, 2021 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Sekta ya elimu katika kipindi cha miaka 60

“leo natoa waraka wa elimu ambao utaelezea ni lini Wanafunzi watakaokatisha masomo kwa sababu ya mimba na changamoto nyingine watapaswa kurejea Shuleni, leoleo natoa waraka hakuna kupoa, zege halilali”

(Visited 23 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us