ASSAs

DIAMOND ANUNUA VITO VYA MILIONI 600

77
0
Share:

Mwanamuziki hodari wa muziki wa bongo fleva na mjasiriamali Nasib Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz ameweka wazi kumiliki vito vipya  vyenye thamani ya zaidi ya Milioni  600.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond ameweka picha kadhaa zinazoonesha baadhi ya sehemu za mwili wake hasa mikono ikiwa imepambwa kwa vito hivyo vya thamani ambavyo ni Pete zilizoenea kwenye vidole vyake vyote vya mkono zikiwa na maneno yenye kusomeka ‘Simba’.

Ambapo ameweka bayana kuwa imemgharimu kiasi cha pesa kisiachopungua Usd 100k ambazo ni sawa na Tsh milioni 230, kununua pete alizovaa pekee, huku Bracelate (Bangili) zikiwa zimemgharimu Usd 117k  sawa na Milioni 407 za Kitanzania.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii Diamond kuonyesha Vito vya thamani ambavyo amekuwa akinunua, mara ya mwisho ni takribani mwezi mmoja uliopita alipoonyesha Saa yake mpya aina ya Rolex yenye thamani ya dola za Kimarekani 30k ambazo ni sawa na Tsh milioni 69.

(Visited 17 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us