ASSAs

SIFA HIZI ZINAIFANYA Infinix NOTE 11 pro KUWA SIMU BORA KWA MWAKA HUU WA 2021.

63
0
Share:

Naitambulisha kwako simu yakufungia mwaka. Hii ni Kwa mujubi wa tovuti mbalimbali za tech kama Tanzaniatech, Teknokona n.k zikijaribu kutuelezea namna teknolojia ya simu inavyoweza kurahisisha kazi mbalimbali.

Katika chambuzi zinazofanywa na hawa watu mimi nimetokea kuvutiwa zaidi na simu aina ya Infinix NOTE 11 pro lakini kabla sijaanza kuichambua hii simu naomba nikuulize je wewe ni mtumiaji yupi wa simu kati ya hawa wawili yule mwenye kuangalia sifa za simu ni namna gani zitaweza kukidhi mahitaji yake katika swala la kujitafutia kipato au ni yule wakutaka kujionyesha tu kuwa anatumia simu ya gharama?

Infinix NOTE 11 pro naweza sema ni zaidi ya simu ikija kwenye swala la uchakataji kazi mbalimbali kama za kiofisi na nyenginezo simu hii inatumia Mediatek Helio G96 processor ni Android ya kwanza kufikia Mediatek Helio G96 najua nyengine zitakuja lakini hii haimaanishi tusiipe kampuni hii sifa yake.

Pamoja kwa kuwa simu yenye processor mahiri kabsa lakini pia simu hii ina features nyengine zenye kuchangia simu hii kuweza kufanya mengi kwa speed ile ile na kwa muda mfupi na features/sifa hizi ni ongezeko la kiwango cha kuirefresh simu kila baada ya matumizi ambayo rate yake ni 120Hz, 

ongezeko la Ram hadi kufikia GB11 pale GB8 inapozidiwa na Monster Game kit ambayo kazi yake kuu ni kuilinda simu isizidiwe wakati wa kuendesha programs zenye ujazo kama za games na yenginezo.

Tukiongelea muonekana wa nje, eneo la nyuma juu kidogo pamependezeshwa na camera pamoja na tundu moja la flash

camera za simu hii ni Megapixel 64+13+2 na eneo la mbele limetawaliwa na wigo mpana wa kioo cha inch 6.95 na camera ya Megapixel 16.

Camera ya Infinix NOTE 11 zinauwezo wa kukivuta kitu kwa ukaribu kwa mara 30X kitaalamu tunaita zoom lens na kisha ndio ukapiga picha pasipo kupungua ubora wa picha lakini pia pasipo kusahau kamera za simu hii zinatumia teknolojia ya AI na cha ajabu zaidi teknoloji hii inauwezo wa kujiswitch kulingana na mazingira pasipo kukomandi. Hapa kwenye kamera najua nitakuwa nimewagusa zaidi wafanyabiashara mtandaoni.

Ni nani anaenunua simu pasipo kuulizia uwezo wa battery, bwana Infinix NOTE 11 pro ina mAh5000 na Wh33 za kuigiza chaji ambayo ni fast chaji kwa matumizi ya kawaida Infinix NOTE 11 pro inachukua siku mbili na ziada kuisha lakini pia ndani ya dakika 45 inajaza battery kwa asilimia 100%.

Infinix NOTE 11 pro inatumia mfumo wa XOS Android 11 ambayo ni Android latest iliyopo kwenye simu nyingi. Haliyakuwa na processor yenye kasi lakini bado ubora unaongezwa na ufanyaji kazi wa Android 11 na kumfanya mtumiaje aepukane kero za kuscroll hadi kupata maumivu ya vidole.

Infinix NOTE 11 PRO inanafasi kubwa ya kutunza kumbukumbu kitaalamu inafahamika kama Memory. NOTE 11 pro ina memory ya GB128 ambayo kazi yake kubwa ni kuhifadhi mambo muhimu kama picha, video, vitabu, miziki n.k

Simu hii inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania ikiwa na ofa ya GB 96 za internet https://www.infinixmobility.com/

(Visited 24 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us